MAHUBIRIMATUKIOWAIMBAJI

Ushuhuda: Ellen Singers walifika Mkoani Simiyu, kisukuma ndio lugha ilifanya kazi yao ya injili kuwa nyepesi.

Waimbaji wa nyimbo za injili toka kikundi cha Ellen SIngers toka Dsm lakini chimbuko lao likiwa ni Bariadi mkoani Simiyu, walifika Mkoani Simiyu kwa kusudi la injili, nao walifanikiwa kufikia jamii kubwa ya watu na kutupa ushuhuda huu.;-

Tulitembelea nyumba karibu 300 na watu wengi walivutiwa sana na uchangamfu wa waimbaji wa Ellen na kwa vile Ellen ni wasukuma, mawasiliano yalifanikiwa sana na hapa ni pale tulipokuwa tunawapa habari za Yesu na kuwaalika kwenye mkutano. Tulikuwa na kadi maalum za mwaliko 500, hii nayo iliwagusa wengi. Walijiona tumewaheshimu sana.

Kuna akina bibi wawili waliwasilisha vifaa vyao vya uchawi, zikiwamo ngozi za fisi na tukazichoma moto na kuwabatiza.”

WEKA MAONI YAKO HAPA
Tags
Show More

Injilileo

Fahamu mengi juu yetu hasa habari za injili, matukio mbalimbali pia shiriki kwa kututumia habari kila siku.
Close