MAFUNDISHOMAHUBIRIMATUKIOWAIMBAJI

Waimbaji wa Ellen Singers toka DSM wamemaliza mkutano wa injili mkoani Simiyu, wamewajengea kanisa waliobatizwa kwenye mkutano huo

Kazi ya utume ni moja ya jukumu kubwa Bwana alilotuachia hapa duniani, waimbaji wa kikundi cha Ellen Singers toka jijini DSM walipata fursa ya kudhamini mahubiri haya yaliyofanyika katika mkoa wa Simiyu, pamoja na mambo mengine waliweza kutoa huduma ya uimbaji na kusaidia kazi ya injili.

Msemaji wa kikundi Dr. Pendo Malangwa aliongea na injilileo na kusema haya;-

“Shalom mpendwa! Asanteni kwa maombi yenu kwa ajili ya Effort ya Ellen Singers- Simiyu. Tunamshukuru sana Baba wa mbinguni kwa kujitwalia mateka zaidi ya 170. Tumehitimisha kwa kishindo kikuu na tulitembelewa na Mkurugenzi wa Global Mission, SNC. Ndoa 6 zilibarikiwa na kupewa vyeti, Bwana ni mwema! Tuzidi kuwaombea ili wadumu na kuleta wenzao wengi. Tumewajengea kanisa la muda na kuwapatia walezi watatu.”

WEKA MAONI YAKO HAPA
Tags
Show More

Injilileo

Fahamu mengi juu yetu hasa habari za injili, matukio mbalimbali pia shiriki kwa kututumia habari kila siku.
Close