MAHUBIRIWAIMBAJI

Waimbaji wa The Healing Voice walishiriki kwenye mahubiri ya TMI 2017, wanao ushuhuda huu baada ya mahubiri haya

Waimbaji wa The Healing Voice wakitokea jijini Dar Es Salaam katika kanisa la Ushindi SDA, nao pia walishiriki kwenye huduma ya kazi ya injili kwa pamoja yaani TMI (Total Member Involvement) na huu ndio ushuhuda wao mara baada ya huduma yao kufanyika.

USHUHUDA BAADA YA TMI.
Tunamshukuru Mungu Kwa kusimamia Kazi yake ya TMI iliyokuwa ikiendelea nchini.
kwa upande wetu kama Healing Voicetz tumeshuhudia mkono wa MUNGU ktk kazi yake, tuwapo shambani mwake Bwana nykati wa TMI. Kwa ufupi, Kanisa Letu la USHINDI lilitutuma kwenda kuhdumu katika kituo cha MASAKI, kutokana na kazi kubwa ya kuamka asubuhi na kuanza kualika watu na kutembelea nyumba kwa nyumba ilibidi Tupige kambi maeneo hayo kwa wiki zote mbili. Kwa wiki ya kwanza kazi ilifanyika vizuri huduma zote ziltolewa zikiwemo za Afya kwa jamii, Muhutubu Mkuu alikuwa PR. DAVID CHIMWASO kutoka Nchi ya CANADA, Mtafsiri MR Nyando Adam toka MAgomeni kaya na Familia, Afya DR MARWA, kwaya na team ya ualikaji ilikuwa Healing Voicetz, lkn wiki ya pili Tulizuiliwa na serikali kwa sababu sauti za mahubiri hayo zilikuwa zikisababisha kelele kwa wakazi wa eneo lile. kwa busara na hekima zaidi, wazee viongozi wa kanisa walifanya mazungumzo na kuomba msaamaa bila mafanikio, kwa masikitiko makubwa tuliondoa vitu vyote TMI kwa MASAKI ikawa imeishia hapo. mioyo yetu iliendelea kuumia sana, Usiku yake tuliomba sana baada ya hapo tulisikia sauti ya YESU ikituita turudi eneo lile,kuna mavuno, KESHO YAKE TULIAMUA KURUDI KUANZISHA DARASA CHINI YA MTI, ili kumaliza kazi ya MUNGU. Darasa ilianza Rasmi na Mhubiri mkuu akawa MWL Lucas Bwirw Manyuru, Afya DR Eugene Moses, Mratibu Barack J Ogillo, Chakula Martha Nyanyama Mkama, kwaya Healing Voicetz, Viongozi wa kanisa walituunga mkono na kuendelea kutuudumia kwa chachula ,Malazi, na usafiri, hivyo basi, wote kwa pamoja tuliuona mkono wa Mungu ktk kazi yake. vitabu vilivyotuongoza ktk masomo hayo ni kitabu cha BIBLIA YASEMA na Biblia Takatifu, Mwisho wa kazi ya TMI Watu 12 Walisikia Sauti ya Yesu na Kubatizwa. JINA LA BWANA LIIMIDIWE. Tazama kwa Picha .

WEKA MAONI YAKO HAPA
Tags
Show More

Injilileo

Fahamu mengi juu yetu hasa habari za injili, matukio mbalimbali pia shiriki kwa kututumia habari kila siku.
Close