Friday, December 09, 2016

   Kikundi cha uimbaji cha Born to Praise kimeanza mwaka 2012 hadi leo kinaendelea na huduma ya uimbaji, wafahamu waimbaji wa kikundi hiki hapa hapa @injilileoblog
Na leo tutakuwa Bambino****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
 
Mwandishi amejadili pia juu ya yale ambayo mwanadamu yeyote, haidhuru awe katika hali gani, akiyafanya atakuwa na sifa ya kuondolewa katika ulimwengu huu wa adha na kuishi katika ulimwengu usio na hata chembe ya taabu. Kundi linaloishi duniani hata leo bila hofu yoyote ya chochote kwani limewekwa huru.

Pendo Lisilo Kifani inakupatia Muonjo wa Wakati Taabu Itakapokoma.  Kwa kusoma kitabu hiki unawezeshwa kuona japo kwa mtupo wa jicho aina ya maisha katika ulimwengu wa raha usiokuwa hata na chembe ya taabu. Maelezo ya mwandishi yanastaajabisha sana.

Ni shauku kuu ya mwandishi kwamba kwa kukisoma kitabu hiki ujue namna ya kuishi kwa tumaini na amani katika ulimwengu huu wa shida, lakini zaidi kwa kufuata maelekezo yake uwezeshwe kuishi kwa namna ambayo utakuwa na sifa za kuishi katika ulimwengu ule usio na taabu wala shida.

Hiki ni kitabu ambacho kwa hakika kila mwanadamu aliyewahi kupata taabu yoyote anakihitaji sana.  Kwa bei ya shilingi elfu mbili tu utapata nakala hii ya ajabu.  Tafadhali dhihirisha pendo lako kwa wanafamilia na marafiki zako kwa kuwanunulia nakala kila mmoja wao nawe utashangaa jinsi watakavyo neemeka.


Maelezo na
Mchungaji Ezekiah Chaboma.
Meneja usambazaji wa vitabu  

Kanisa la waadventista wa Sabato, Union ya kusini mwa Tanzania.****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, December 08, 2016


Miongoni mwa maswali yanayoulizwa na wengi leo ni juu ya hali ya kusikitisha ya Dunia yetu. Je tumefikaje huko? Hali hii ya Uovu ilianzaje? Wako wengi waliojaribu kutoa majibu lakini yaliyojengwa katika Sayansi na Falsafa. Hata hivyo yanatofautiana sana na kushindwa kukidhi hasa hitaji lenyewe, na kuibua swali jipya kabisa; Ni wapi basi tutapata ukweli halisi?

Kitabu cha Pendo Lisilo Kifani, ambacho kimsingi kimejengwa katika Maandiko Matakatifu, yaani Biblia, kimesheheni majibu ya kweli halisi ya maswali yanayohusiana na mstakabali wako na wa Dunia hii.

Mwandishi, kwa karama ya Mungu, anaeleza juu ya Mwanzo ambao ulikuwa mkamilifu usio na kasoro au dhambi, maelezo ambayo kwa hakika yanagusa sana hisia.

Utashangaa kusoma jinsi dunia hii ilivyokuwa mara baada ya kuumbwa, mwanadamu wa kwanza akikutana na kuzungumza na Mungu katika mazingira mwanana kabisa, yenye maua, mito, wanyama, na ndege wa namna namna.

Ile siri ya Uovu kuibuka ndani ya kiumbe mkamilifu imejadiliwa kwa kina.  Hata hivyo kinachogusa zaidi ni jinsi Mungu alivyofanya hima kuwatahadharisha Adamu na Hawa ili wasiingie dhambi, na zaidi sana kile alichofanya kwa gharama kubwa kuhakikisha kwamba njia inapatikana ya kumtoa Mwanadamu katika dhambi na athari zake na kuikomesha taabu kabisa.  Uajabu wa Pendo lisilo kifani uliodhihirishwa katika kifo cha Yesu, ndio hasa kiini cha kitabu hiki, utafurahi na kunufaika sana kusoma kisa hiki cha ajabu cha kumwokoa mwanadamu.


 Maelezo na
Mchungaji Ezekiah Chaboma.
Meneja usambazaji wa vitabu  

Kanisa la waadventista wa Sabato, Union ya kusini mwa Tanzania.


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Wednesday, December 07, 2016
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Monday, December 05, 2016


Donald Trump amemteua mmoja wa washindani wake kuwa Waziri wa makazi na ustawi wa miji.
Rais huyo mteule amesema amefurahishwa sana kumteuwa Dkt. Ben Carson ambae amemtaja kama aliye na uwezi wa kuimarisha masuala ya jamii.
Ben Carson alistaafu kama daktari wa upasuaji wa kichwa.
Mwandishi wa BBC mjini Washington Marekani amesema bwana Trump na Carson wananuia kuwavutia wafuasi wa chama cha Republican ambao wametaka uwongozi uwepo kwa watu wasio ya uzoefu wa kisiasa.
Dkt Ben Carson ana ushawishi mkubwa miongoni mwa Wamarekani wa madhehebu ya kiinjilisti.

Habari na BBCSWAHILI
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
  Na Andrew McChesney
Waadventista Wasabato walijiunga ya maelfu ya watu katika uwanja wa Chapecoense  Brazil kuomboleza wale waliouawa katika ajali ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji wa mpira wa soka, na kushiriki matumaini yao katika ufufuo wa wafu pale Yesu anaporudi Mara ya Pili.Jumla ya watu 71 walikufa wakati ndege iliyokuwa imebeba timu ya soka ya Chapecoense na kupata hitirafu Novemba 28 karibu na Medellin, Colombia. Watu sita walinusurika. ndege iliishiwa ya mafuta muda mfupi kabla ya ajali. Majeneza kadhaa yaliwasili katika uwanja wa timu ya nyumbani wa Chapeco, mji wenye watu 210,000  kusini mwa Brazil siku ya Jumamosi.Washiriki wa kanisa walisimama katika mvua kusambaza maelfu ya nakala za kitabu "Only Hope" - "Tumaini Pekee" na muinjilisti wakiadventista Alejandro Bullon alifundisha kama vile lebo ya kwenye chupa ya maji ilivyokuwa imeandika ahadi ya Ufunuo 21: 4, "Na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao; kutakuwa na kifo tena, wala maombolezo, wala kilio. Kutakuwa na maumivu tena, kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita "(NKJV)."Ilikuwa ni mvua, lakini maelfu ya washiriki wa kanisa walitoka nje na vitabu, maji, na kadi na kuvigawa," alisema Magdiel E. Pérez Schulz, msaidizi wa rais wa kanisa la Wasabato dunia, ambaye amekuwa akiwasiliana na washiriki wa kanisa kanisa mahalia. "Washiriki wa kanisa pia wakaomba pamoja wale wanaohudhuria mazishi na kupata kukumbatiana kwa ishara ya matumaini."
 Habari kamili BOFYA HAPA


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Rai imetolewa Kwa Waamini Wote wa Kanisa La Waadventista wa Sabato Kupeleka Injili Kwa Jamii zote, Dini zote, na Madhehebu.
Rai hii imetolewa na Pr. Godwin Lekundayo Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo Kuu la Kaskazini Mwa Tanzania wakati akitoa somo la Ufunguzi wa Vipindi vya Leo tarehe 05/12/2016 katika Mkutano wa East Central Africa Division AMR/AM CONGRESS unao endelea Hapa Kongowe Adventist Primary School December 04-10, 2016.
THEME: MISSION POSSIBLE.
MOTTO: CROSS-CULTURAL IS OF THE GREATEST NEED OF THE HOUR
WAHUSIKA: WACHUNGAJI NA WALEI KUTOKA NCHI 11 ZA AFRIKA ZINAZO UNDA DIVISION YA ECD.
 
 
Image may contain: 4 people
BWANA YESU atukuzwe ndugu zangu wote.
Karibuni tujifunze Neno la MUNGU.
Kusudi la MUNGU ni wewe uoe au uolewe na wa kufanana na wewe.
Sio kufanana sura au nywele au pua bali kufanana utakatifu sahihi.
Wewe ukiwa mtakatifu na MUNGU atakupa wa kufanana na wewe yaani atakupa mtakatifu kama wewe ulivyo mtakatifu.

Mwanzo 2:18 '' Bwana MUNGU akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.''
Mke au Mume wa kufanana na wewe anapatikana kwa MUNGU tu.
Kama wewe huishi maisha matakatifu basi MUNGU hatakupa ila utajichagulia wewe.
Mimi Peter nimeyapitia maisha ya ujana ndio maana nafundisha vijana kwa habari ya Mchumba.
Katika maisha yangu ya kabla sijaoa nimewahi kujulishwa na mabinti 4 kila mmoja kwa wakati wake kwamba amefunuliwa kuhusu mimi kwamba nitamuoa lakini mtu niliyekuja kumuoa ni yule aliyekuja kufunuliwa baadae sana baada ya mimi kufunuliwa.
Kwanini ninayasema haya?
Ndugu, MUNGU huwafunulia watu wake lakini pia shetani naye ana uwezo wa kuwafunulia watu watu wa MUNGU ili waende nje na kusudi la MUNGU.
Si kwamba hao waliofunuliwa kuhusu mimi hawakuwa watu waliookoka na wanaishi maisha matakatifu, ila sio kila mtakatifu ni wa kwako bali kutoka katika kundi la watakatifu MUNGU atakupa aliye wako.
Hivyo ndugu yangu ambaye hujaoa au kuolewa nakuomba tena nakuomba sana sana kwamba Mchumba wako usimthibitishe kupitia ndoto tu bali mthibitishe katika utakatifu na kumcha MUNGU, Tena mthibitishe katika nia ya KRISTO ndani yake.

Kuna Ndoto za aina tatu(3).
1. Kuna ndoto kutoka kwa MUNGU.
Mwanzo 20:6 ''MUNGU akamwambia katika ndoto, Nami nimejua ya kwamba kwa ukamilifu wa moyo wako umefanya hivi, ndipo nami nikakuzuia usinitendee dhambi, kwa hiyo sikukuacha umguse.''
2. Kuna ndoto huletwa na shetani
Zakaria 10:2 '' Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji.''
3. kuna ndoto kutoka kwako mwenyewe kupitia yale ambayo yameujaza moyo wako muda wote.
Mhubiri 5:3 ''Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.''
Leo sifundishi ndoto maana nimewahi kufundisha sana kuhusu ndoto ila nataka nikupe angalizo kidogo kama wewe huwa unataka mpaka uote ndoto ndipo ujue umepewa Na MUNGU huyo Mchumba wako.
Kwa sababu kuna aina tatu za ndoto, Je ndoto uliyoona wewe kuhusu mwenzi wako unadhani imetoka kwa MUNGU?
Sio ndoto zote hutoka kwa MUNGU ndio maana unatakiwa uwe makini sana.
Kuna Ndoto hutoka kwa MUNGU lakini zikionyesha jambo lisilotoka kwa MUNGU ili tu kukufundisha wewe ujue na ujue namna ya kuomba, Hivyo anahitajika sana ROHO MTAKATIFU ili kukusaidia kujua, na ROHO MTAKATIFU huwezi kumpata kama hujaokoka.
Kuna Ndoto hutokea kwa sababu ya kuwazia sana jambo hilo utajikuta unaota ndoto na kwa sababu unampenda mtu huyo basi hapo hapo utaweka muhuri kwamba ni MUNGU amesema na wewe kumbe ni ufahamu wako unakudanganya.
Ni kweli kabisa MUNGU husema sana na watu wake kwa njia ya ndoto lakini naomba ujue kwamba hata shetani naye huleta ndoto na hata mawazo yako yanaweza kuzaa ndoto hivyo uwe makini sana na sio ndoto tu ndio iwe kithibitisho chako cha kwamba huyo uliyemuota ndio anafaa kuwa mke mwema wako au mume mwema wako kutoka kwa MUNGU.
Ukiota ndoto naomba uwaze mambo yote matatu ili ujue jinsi ya kumuomba MUNGU na ili upate kitu sahihi.
Kuna watu walipendana tu na kuoana na wanaishi maisha mazuri sana kwa sababu ndoa hiyo ni mpango wa MUNGU, sasa wewe unayesubiri ndoto naomba ujue na hilo pia.
MUNGU anaweza akasema na wewe kupitia upendo tu wa utakatifu.
MUNGU anaweza akasema na wewe kwa ishara na pia MUNGU anaweza akasema na wewe kwa kupitia watu wengine, tena MUNGU anaweza akasema na wewe kwa mazingira tu, hivyo usitarajie MUNGU aseme na wewe kwa ndoto tu.
MUNGU ana njia nane za kibiblia za kusema na watu wake na tena MUNGU anaweza akasema na wewe kupitia njia hata zaidi ya hizo njia nane za kibiblia.
1 Kor 7:2 '' Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.''
Kipimo kikuu cha mtu sahihi kwako ni kama mtu huyo anamcha MUNGU katika KRISTO YESU na anamwabudu katika Roho na kweli.
Lakini pia naomba ujue kwamba kama wewe huishi maisha matakatifu basi wewe mwenyewe pia hufai kuwa mke mwema au mume mwema hivyo hata suala lako la kutaka mke mwema au mume mwema kutoka kwa MUNGU lifute kwanza maana halikuhusu , hadi utakapompokea Bwana YESU kwa upya na kuanza kuishi maisha matakatifu.
Kuna watu husubiri mpaka wafunuliwe ndipo waoe au waolewe.
Ndugu shetani anaweza akakuwahi mapema sana na kukufunulia ukidhani ni MUNGU anakufunulia, lengo tu upishane na kusudi la MUNGU.

Kama Binti ni mcha MUNGU ukimpenda bila hata kufunuliwa na ukawa na amani kwake huyo anakufaa kuwa mke mwema wako.
Kama kijana ni mcha MUNGU na akakujulisha kwamba anataka kukuchumbia kama jambo hilo litapata amani moyoni mwako huyo ni mume mwema wako, sio mpaka uoteshwe ndoto ndugu.

Pia katika kuwa na amani na mtu unatakiwa uangalie kwamba una amani kwa sababu ya nini? na huna amani kwa sababu ya nini?
Kama una amani na kijana huyo kwa sababu tu ana elimu na ana gari basi hiyo ni amani feki.
Kama huna amani na kijana kwa sababu tu hana hela na hana kazi nzuri basi huko sio kutokuwa na amani bali ni tamaa inakutesa.

Waebrania 13:4-5 '' Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu. Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa.''
Kuna waigizaji pia hivyo inabidi uwe mtu wa maombi sana ndipo utajua ni nani ana mcha MUNGU na ana hofu ya MUNGU ili akufae maishani mwako kama mwenzi wako wa ndoa takatifu.
Mtu ambaye yuko moto kiroho utamjua tu kama ana mcha MUNGU kisawasawa.
Anayemcha MUNGU kisawasawa huyo ndiyo yuko moto kiroho, tena huyo ndiye aliyekua kiroho kuliko hata yule mtu mwenye cheo kanisani na ana miaka zaidi ya 20 Kanisani lakini hamchi MUNGU.
Inabidi uwe makini sana katika kuchagua mwenzi.
Mithali 16:6 ''Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu.''
Usimthibitishe mchumba wako kwa ndoto tu labda kama umethibitisha ni MUNGU amesema na wewe.
Asante kama umelielewa Neno la MUNGU ila nina neno moja la mwisho kwako leo.
BWANA YESU Amekaribia Kurudi.
Je, Umejiandaaje?
Je, Unaendeleza Dhambi Ili Siku Ile Uachwe Na BWANA YESU? Je, Umeshika Wokovu Na Utakatifu Hata Unyakuliwe Siku Ile Kwa Ajili Ya Kwenda Uzima Wa Milele?
Majibu Sahihi Yako Moyoni Mwako Ila Nakusihi Mpokee BWANA YESU Kama Hujampokea Na Nakusihi Ishi Maisha Matakatifu Ukiwa Ndani Ya Wokovu.
Vya Dunia Tulivikuta Na Tutaviacha.
Ndugu, Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Kuokoka.
Vya Dunia Visikupotezee Muda Wako Hata Ukasahau Wokovu Wa BWANA YESU Kwako.
Ni mimi ndugu yako Peter M Mabula.
Mtenda kazi katika shamba la BWANA YESU.
0714252292.
mabula1986@gmail.com
Ubarikiwe sana kwa kusoma somo hili          ****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Friday, December 02, 2016

FUNGU KUU: YOHANA 1:14
SOMO: AMEJAA NEEMA NA KWELI
MUHUBIRI: MCHUNGAJI EMMANUEL RAJABU
UIMBAJI: KWAYA YA KANISA NA YA VIJANA KIJICHI
WOTE MNAKARIBISHWA

 
****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
   Kikundi cha uimbaji cha Born to Praise kimeanza mwaka 2012 hadi leo kinaendelea na huduma ya uimbaji, wafahamu waimbaji wa kikundi hiki hapa hapa @injilileoblog
Na leo tutakuwa nae Suzanne


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***

Thursday, December 01, 2016

Siku maalum ya kuhamasisha kununua nakala nyingi za kitabu cha PENDO LISILO KIFANI ili kuwafikishia ujumbe watu wengi kwa njia ya vitabu, imefanyika jumamosi iliyopita katika kanisa la Waadventista wa Sabato Ushindi ikishirikisha wainjilisti mbalimbali toka kanda zote za Dar na Pwani.Mgeni akiwa ni mwenyekiti wa Union ya Kusini mwa Tanzania Mch. Mark W. Malekana.


 Picha/Habari na Chabo Maphoto


****TUMA PICHA NA VIDEO WhatsApp 0713 059 073 NA 0717 367 693***
Blogger Widgets

SIKILIZA NA DOWNLOAD WIMBO "AYUBU" WAIMBAJI IMBA KWA AKILI CHOIR